Kanisa Hai la Mungu

Mpango wa Miaka 7,000 wa Mungu

Mungu aliumba Dunia mabilioni ya miaka mingi iliopita, lakini aliumba wanadamu wa kwanza, Adamu na Hawa, kama miaka 6,000 iliyopita. Biblia inatufafanulia wazi kipindi chetu cha miaka 6,000 cha sasa, ambacho kiasi kikubwa cha wanadamu kinafuata fikira zake tofauti na za Muumba. Kipindi hiki cha miaka 6,000 kitafuatwa na utawala wa miaka elefu moja wa Yesu Kristo duniani, ambapo Kristo na watakatifu waliofufuliwa watafunza ulimwengu mzima njia za kweli za Mwenyezi Mungu. Taarifa: “ Wameneemeka sana, tena heri yao wote wanaoshiriki ufufuo huu wa kwanza. Kifo cha pili hakitakuwa na nguvu juu yao; watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, na watatawala pamoja naye kwa miaka elfu moja ” (Ufunuo 20:6). 

Wayahudi wa nyakati za Yesu walielewa vyema dhana ya siku za wiki kuwa mfano wa miaka elfu moja katika Mpango wa Mungu. Petro alieleza kanuni hii: “Lakini, wapenzi wangu, msisahau kitu kimoja! Mbele ya Bwana, hakuna tofauti kati ya siku moja na miaka elfu; kwake yote ni mamoja” (2 Petro 3:8). Kwa hivyo, wiki ya siku saba inasawiri mpango wa miaka 7,000 wa Mungu, siku sita za wiki zikisawiri wakati huu wa jamii ya binadamu ya sasa, zitakazofuatwa na miaka elfu moja ya utawala wa Kristo akiwa kama Mfalme wa Wafalme (Ufunuo 11:15).

Edward Gibbon aliandika katika historia yake maarufu ya dunia, The Decline and Fall of the Roman Empire (Kudhoofika na Kuangamia kwa Ufalme wa Warumi), “ Mafundisho ya kale na ya umma ya Milenia yalikuwa yamenugana kwa ukaribu kabisa na kuja kwa pili kwa Kristo. Kwa kuwa kazi za kuumba zilitimizwa baada ya siku sita, kuwepo kwake katika muundo huu wa sasa ulipangwa kuwa wa miaka elfu sita, kwa kufuatana na desturi ambayo inasemekana ilitajwa na nabii Elijah. Na kwa analojia hiyo hiyo inasemeka kwamba kipindi hiki kirefu wa kazi na mabishano, ambacho sasa kinakaribia  kuisha, kitafuatwa na Sabato ya furaha ya miaka elfu moja; na kwamba Kristo, na kundi la ushindi la watakatifu na waliochaguliwa ambao wamekwepa kifo, au ambao wamefufuliwa kwa muujiza, wata tawala duniani hadi wakati uliopangwa wa ufufuo wa mwisho na wa ujumla” (toleo, 1, uk. 403).

Baada ya Milenia, Mungu ataongoza Hukumu ya Enzi Nyeupe , iliyoelezwa katika Ufunuo 20. Binadamu wote ambao waliishi na kufa bila kusikia Injili ya kweli watapewa fursa kukubali dhabihu ya Yesu Kristo, kupokea Roho Mtakatifu na kujifunza kuishi katika njia ya Mungu. Wale ambao wamemkubali Kristo watakuwa moja na Familia ya Mungu milele na wale watakaomkataa watapata mauti ya milele katika Ziwa la Moto (Ufunuo 21:8).

Kujua zaidi juu ya Milenia na nyakati zijazo, tafadhali soma kijitabu chetu, Dunia ya Siku za Mbeleni: Kutakuwaje?


Copyright © 2009 Living Church of God
swahili.lcg.org