Kanisa Hai la Mungu

Sabato za Kila Wiki na za Mwaka

Biblia ina funua kwamba “siku ya saba ni Sabato ya Mungu” (Kutoka 20:10;     
Kumbukumbu la Torati 5:14). Ina paswa kuadhimishwa kuanzia machweo ya Ijumaa hadi machweo ya Jumamosi. Ni “ishara” ya Mungu katika Yake na Waumini wake  ikionyesha “mapumziko” ya Mungu na kutukumbusha kuwa Yeye ni Muumba. Inaonyesha pia Milenia, kuja kwa “mapumziko” ya miaka 1,000 wakati Kristo atakaporudi kama Mfalme wa Wafalme (Waebrania 4: 1-4; Ufunuo 20:4-6). Daima Yesu Kristo, Watume na Kanisa la mwanzoni walifuata amri ya Mungu ya Sabato, (Luka 4:16, Matendo ya Mitume 17:2), na itaadhimishwa na “mwili wote” wakati wa kuja kwa utawala Kristo duniani wa millennia (Isaya 66:23).
         
Tamasha za kila mwaka za Mungu zimeorodheshwa katika Walawi 23 na Kumbukumbu la Torati 16. Hizi siku takatifu zilizotolewa na Mungu ziliamuriwa kuadhimishwa “milele” (Walawi 23:14, 21, 31, 41). Kanisa la Karne-kwanza liliadhimisha Sabato za kila mwaka (Matendo ya Mitume 2; 12:3-4; 18:21; 20:6, 16; 27:9; 1 Wakorintho 16:8). Sabato hizi zitaendelea kuadhimshwa wakati wa utawala wa Kristo wa Milenia (Zekaria 14:1, 9, 16-19)

Tamasha za Mungu za kila mwaka zinaonyesha hatua saba muhimu katika mpango Wake wa wokovu:

1. Pasaka ya Wayahudi inaonyesha dhabihu ya Yesu Kristo, “Mwana kondoo wa Mungu” (Yohana 1:29, 36; Ufunuo 5:6) iliyotolewa kwa ajili yetu, (1 Wakorintho 5:7). Yesu alianzisha Pasaka ya Agano Jipya kwa ishara ya mkate na divai (1 Wakorintho 11:23-26).

2. Siku Saba za Mkate usiowekwa chachu ni ashiria ya kutakasa uchachu wa uovu na dhambi kwenye maisha ya muumini, na kushiriki katika asili ya Mungu, “mkate usiowekwa chachu wa uaminifu na ukweli” (1 Wakorintho 5:6-13; Luka 12:1)

3. Sherehe ya Mazao ya Kwanza (Pentekoste) inaonyesha vuno dogo la “lililozalishwa” la wafuasi wa Kristo ambao watavunwa wakati “ufufuo wa kwanza” (Ufunuo 20:4-5), kama  “aina ya mazao ya kwanza” (Yakobo 1:18).
4. Sherehe za Tarumbeta zinatabiri kuja kwa mara ya pili kwa Yesu Kristo, wakati wa mlio wa tarumbeta wa saba, baada ya kipindi cha vita na migongano ya nyakati za mwisho (Mathayo 24:31; 1 Wakorintho 15:52; 1 Wathesalonike 4:13-17; Ufunuo 11:15-18; 19:15; Zekaria 14:9).

5. Siku ya Upatanisho inaonyesha kufukuzwa kwa Shetani, na kufika kwa mwanadamu  katika amani ya Mungu (Mambo ya Walawi 16:8, 10, 15-27; Ufunuo 20:1-3).

6. Sherehe ya Tabenakulo inaonyesha ulimwengu unaokaribia kuja utakaokuwa chini ya uongozi wa Yesu Kristo na watakatifu Wake (Zekaria 14; Mathayo 9:37-38; 13:1-30; Luka 12:32; Yohana 7:6-14; Matendo ya Mitume 17:31; Ufunuo 12:9; 20:4-6).

7. Siku Kuu ya Mwisho ina onyesha hukumu kuu itakayofanyika mwishoni mwa utawala wa millennia wa Yesu Kristo duniani (Yohana 7:37; Mambo ya Walawi 23:36, 39, 33-34; Ufunuo 20:11-12).

   Kujua zaidi kuhusu mada hii, tafadhali soma kijitabu chetu, Siku Takatifu: Mpango Mkuu wa Mungu

Copyright © 2009 Living Church of God
swahili.lcg.org