Kanisa Hai la Mungu

Asemavyo Mungu Kuhusu Siku Zako Zijazo

Mungu aliumba binadamu kutoka kwenye “mavumbi ya ardhi” (Mwanzo 2:7). Wanadamu wameumbwa katika “mfano [na] sura ” (Mwanzo 1:26; cf. 5:3); pia wamepewa akili na hisia ya kiMungu. Mungu alipanga kwamba wale wanaotubu dhambi zao na kubatizwa watapokea Roho wa Mungu (Matendo ya Mitume 2:38-39; Yohana 3:16). Kuja kwa pili kwa Kristo, wale wote waliookoka katika maisha haya, wawe hai au wafu, watapewa uzima wa milele, na kuzaliwa kama “watoto wa Mungu kwa vile wamefufuliwa katika wafu” (Luka 20:36).
       
          Heri walio wapole, maana watairithi nchi” (Matayo 5:5; cf. Zaburi
37:9, 11, 22, 29, 34). “Yeyote atakayeshinda atapokea hiki [ulimwengu]” (Ufunuo 21:7).

Kufuatana na unabii na ahadi zote za Biblia, “Mazao ya kwanza” ya Mungu (Walioitwa wakati huu) wata tunukiwa na mahali au nafasi ya uongozi katika Ufalme wa Mungu (Yohana 14:1-3; Ufunuo 3:21; 20:4-6), hapa hapa duniani (Ufunuo 2:26-27; 5:10; Danieli 2:44). Watakatifu wa kweli watakuwa wana kamili wa Mungu, “wana wa ufufuo” (Luka 20:36).  Madhumuni ya Mungu ni kwamba watu wanaokubali dhabihu ya Yesu Kristo na Kumtii wataishia kuwa washirika kamili wa Familila ya Mungu, chini ya mamlaka ya Baba na Mwana (1 Yohana 3:1-3). Watagawana utukufu mtakatifu katika ufufuo. Yesu aliomba, “Utukufu ule ulionipa nimewapa wao, ili wawe na umoja kama Sisi tulivyo wamoja. Mimi ndani Yako na Wewe ndani Yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja na ulimwengu upate kujua ya kuwa umenituma, nami nimewapenda wao kama unavyonipenda Mimi.” (Yohana 17:22-23).

 Kujua zaidi juu ya Mpango wa Mungu unaohusu siku zako za mbeleni, soma kijitabu chetu, Hatima yako ya Mwisho. 

Copyright © 2009 Living Church of God
swahili.lcg.org