Kanisa Hai la Mungu

Kuishi Jinsi Mungu Atakavyo Leo

Ukristo wa kweli ni “namna ya kuishi.” Yesu alinena kwa dhairi kabisa katika Luka 4:4, “Binadamu hataishi kwa mkate pekee, bali kwa kila neno la Mungu.” (Luka 4:4). Biblia sio tu ni mwongozo wa imani yetu ya kila siku; ni neno la Mungu, linaloonyesha jinsi ya  
kuishi ndani ya Mungu, namna ya kupenda, kutoa, na kumtumikia. Kristo anatufundisha kuishi katika hivyo.  Pia, Biblia ni msingi wa elimu ya kweli. Yesu alisema, “…Mtaujua ukweli, nao ukweli utawapeni uhuru” (Yohana 8:32).
 
Utengano huu unamaanisha kwamba wale ambao Mungu amewaita watishi maisha tofauti na wale waliokaribu nao, na kwa namna ya kwel “mabalozi” wa serikali ya Mungu. (Waefeso 6:20; 1 Petro 2:9-10). Wakristo wanapaswa kuwaombea viongozi wa mataifa yao, ambao Mungu amewaweka hapo, lakini katika historia Kanisa la Mungu linafunza washirika wake wasishiriki katika siasa za dunia.

Uponyeshaji mtakatifu ni moja wapo ya manufaa ya kuishi ndani ya Mungu. Uponyeshaji ni moja wapo ya “zawadi za kiroho” (1 Wakorintho 12:1,9). Mojawapo ya Jina la Mungu la Kihibrania ni Yahweh Ropheka, likimaanisha “Mwenye Enzi anayeponya”. Mungu ni Mwenyezi Mkuu anaye “samehe dhambi zako zote, anaeponya magonjwa yako yote” (Zaburi 103:3; 1 Petro 2:24). “Je, yuko mgonjwa kati yenu? Anapaswa kuwaita wazee wa kanisa, nao watamwombea na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Wakiomba kwa imani mgonjwa ataponyeshwa; Bwana atampatia nafuu, na dhambi alizotenda zitaondolewa.
Basi, ungamanianeni dhambi zenu, na ombeaneni, ili mpate kuponywa. Sala ya mtu mwema ina nguvu ya kutenda mengi.” (Yakobo 5:14-16).
 
Kanisa Hai la Mungu linafuata maagizo haya ya moja kwa moja ya bibilia. Tunaamini kwamba Mungu anaponya sasa kulingana na imani ya mtu na mapenzi ya Mungu katika kila jambo. 

Neno la Mungu linaamuru binadamu wote wapende majirani zao kama wanavyo jipenda wenyewe (Walawi 19:18; Mathayo 22:39; Mitendo ya Mitume 17:24-29). Mungu anafunua kwamba wokovu unatolewa wazi kwa Wayahudi na Wasio wayahudi  (Matendo ya Mitume  10:34-35; Warumi 10:12-13; cf. Yoeli 2:32). Tunaamini kwamba upendo na heshima unapashwa uonyeshwe kwa watu wa makabila yote (Warumi 13:10).

            Kujua zaidi juu ya namna maisha ndani ya Mungu yanavyoweza kukuletea amani kuu na
            mafanikio, soma kijitabu chetu, Amri Kumi.

Copyright © 2009 Living Church of God
swahili.lcg.org