Kanisa Hai la Mungu

Kanisa Ni Nini

Jina la biblia la Kanisa la kweli ni “Kanisa la Mungu.” Mungu anataja vitu kama vile vilivyo. Jina lina tajwa wazi kabisa katika asili ya umoja na wingi kwenye sehemu kumi na mbili tofauti katika Agano Jipya, ikijumuisha Matendo ya Mitume 20:28;1; 1 Wakorinto  1:2; 10:32; 11:16; 1 Timotheo 3:15.

Kanisa Hai la Mungu lina Washirika katika nchi nyingi duniani, wenye nia ya kuendeleza Agizo Kuu lililotolewa na Yesu Kristo:

Kuhubiri Injili ya kweli ya Ufalme wa Mungu (Marko 1:14; Mathayo 24:14; Ezekieli 3 na 33), na Jina la Yesu Kristo (Matendo ya Mitume 8:12) katika mataifa yote kama ushuhuda.

Kulisha waumini na kuandaa masharika ya Kanisa ya ndani ya sehemu zote kuweza kugawa mahitaji ya kiroho na  kimsingi ya washirika wetu jinsi Mungu awezeshavyo (1 Petro 5:1-4; Yohana 21:15-18).

Kuhubiri unabii wa mida ya mwisho na kuonya mataifa yanayoongea-Kingereza na ulimwenguni kote duniani juu ya kuja kwa Majonzi Makuu (Mathayo 24:21).

Historia ya Kanisa Hai la Mungu ilianzia katika Kanisa la Kitabu cha Matendo ya Mitume (wakati wa Waefeso) la karne-kwanza, hadi kufikia  sasa. Ujumbe uliotumwa kwa Makanisa saba katika Ufunuo 2 na 3 kwa mfululizo unaonyesha historia ya Kanisa la kweli kutoka wakati huo kuendelea mbele. Makanisa haya saba yanaeleza mfuatano wa nyakati, au enzi, za Kanisa la Mungu. Tuna amini kuwa enzi ya Philadelphia ilianza kwenye miaka1930, na kuwa sisi ni mwendelezo wa enzi hiyo ya Philadelphia.

            Je una tafuta Kanisa la kweli la Mungu? Kujua zaidi, soma kijitabu chetu,
            Kanisa La Mungu La kweli Liko Wapi?

Copyright © 2009 Living Church of God
swahili.lcg.org