Kanisa Hai la Mungu

Kanisa Hai la Mungu ni mwendelezo wa kisasa wa Kanisa lile lile lilliloanzishwa na Yesu Kristo mnamo 31AD, na linalenga kufuata ‘Ukristo wa asili’ ule ule uliofundishwa na Yesu Kristo na watume wake.

Kanisa liko hai katika mabara sita, na lina zaidi ya masharika 300 ulimwenguni. Kwa wakati huu, usambazaji wa habari zetu kwa umma hufanywa hasa kwa Kiingereza, Kifaransa au Kihispania. Tuna tumaini kuwa tovuti hii  itakupa maelezo ya msingi ya ujumla yanayohusu misheni yetu na kututamulisha, ila ili uweze kupata manufaa zaidi ya habari zetu zilizopo hivi sasa, utahitaji kuelewa Kiingereza, Kifaransa au Kihispania, au kutafuta rafiki ambaye anafahamu lugha nyingi anaeweza kukutafsiria habari zetu.

Ikiwa unafahamu Kanisa la Mungu Ulimwenguni la kabla ya1986, ambalo Mungu alilikuza kupitia kwa Bw. Herbert W. Armstrong, unaweza ukawa tayari na ufahamu wa msingi wa dhana na desturi zetu. Mungu alikuza Kanisa Hai la Mungu kupitia kwa Bw. Roderick C. Meredith, mmoja wa wainjilisti wa watano wa kwanza ambao Bw. Armstrong alifanya kasisi mwaka 1952, ili kuendeleza Kazi ya Mungu katika nyakati zinazo tukabili za uasi wa dini na ukanaji. Tunajitahidi kutimiza “Agizo Kuu” ambalo Yesu Kristo alilipa Kanisa lake la kuhubiri Injili ya ukweli ikiwa kama ushuhuda kwa mataifa yote na kulisha waumini waitwao na Mungu. Wainjilisti, wachungaji na wazee wa kanisa kote ulimwenguni wanajitahidi kufanya “uongozi wa utumwa” wa kikweli kweli wakiwa kama wachungaji wapendao watu wa Mungu ambao wanajifunza kufuata Njia ya Mungu maishani mwao.
 
Ili kujua zaidi kuhusu Kanisa, tafadhali bofya mada zifuatazo hapo chini:

Kuhubiri Injili
Kanisa ni nini?
Sabato za Kila Wiki na za Mwaka
Mpango wa Miaka 7,000 wa Mungu
Utume wa Biblia
Kuishi Jinsi Mungu Atakavyo Leo
Asemavyo Mungu Kuhusu Siku Zako Zijazo

Tunasikitika kwamba kwa hivi sasa, hatuna wawakilishi au tuna wawakilishi wachache wanaofahamu lugha yako.  Wawakilishi wetu wengi wanajua Kingereza. Baadhi ya wawakilishi wetu wanajua pia Kifaransa au Kihispania. Hapo mbeleni, tunatumaini kutafsiri baadhi ya habari zetu katika lugha yako. Kutusaidia kujua kiwango cha shauku, tafadhali tujulishe habari gani zaidi za kwetu ungependa kusoma katika lugha yako ya asili. Kwa sasa, tunatarajia utafurahia habari zetu zilizoandikwa kwa Kingereza, Kifaransa na Kihispania.

Kama unataka kuwasiliana na mwakilishi wa Kanisa Hai la Mungu katika lugha ya Kiingereza, tafadhali tuma barua-pepe kwa [email protected], au tupigie simu namba (704) 844-1970, au tuandikie kwa kutumia anwani:

Living Church of God
P.O. Box 3810
Charlotte, NC 28227-8010

Kama unataka kuwasiliana na mwakilishi wa L’Eglise du Dieu Vivant katika lugha ya Kifaransa, tafadhali tuma barua-pepe kwa
[email protected],  au tupigie simu namba (704) 844-1960 x220, au tuandikie kwa kutumia anwani:

Eglise du Dieu Vivant
P.O Box 3810
Charlotte, NC 28227-8010

Kama unataka kuwasiliana na mwakilishi wa La Iglesia del Dios Viviente katika lugha ya Kihispania, tafadhali tuma barua-pepe kwa [email protected], au tupigie simu namba (704) 844-1960 x217, au tuandikie kwa kutumia anwani:

Iglesia del Dios Viviente
P. O. Box 3810
Charlotte, NC 28227-8010

 

 

Kwa maelezo ya ujumla ya kazi hii ya lugha-Kingereza, tazama video hii, ambayo ilionyeshwa wakati wa mikutano ya mwaka ya Sherehe za Tabenakulo ya 2008: Behind the Work 2008

www.wvm.co.za |  www.weltvonmorgen.org |  www.elmundodemanana.org
www.mondedemain.org |  www.wereldvanmorgen.nl

Copyright © 2009 Living Church of God
swahili.lcg.org